1 of 65

Ufundishaji na ujifunzaji wa kutumia mbinu ya onesho mbinu.�

2 of 65

Maana ya onesho mbinu�

  • Onesho mbinu ni njia ya ufundishaji na ujifunzaji ambayo mwalimui hufanya baadhi ya vitendo mbele ya darasa na baadae huwaruhusu wanafunzi kufanya vitendo hivyo(kuiga vitendo vilivyotendwa na mwalimu) hatua kwa hatua.
  • Vitendo vinavyotendwa na mwalimu huwa ni vya hatua kwa hatua ili kukamilisha shughuli mahususi ambayo mwalimu amepanga kukikamilisha katika muda huo.
  • Onesho mbinu inapotumika katika ufundishaji na ujifunzaji wa nadharia kadhaa za kisayansi hufanya dhana kuleweka kwa urahisi hata zile tata.

​

3 of 65

Mambo ya kuzingatia katika mbinu onesho mbinu hii ya �

  • Mambo ya kuzingatia katika mbinu onesho mbinu hii ya
  • Kuandika maelezo mafupi ya wazi yanayohusiana na kile kitakachotokea .
  • Maandalizi ya vifaa vitakavyotumika
  • Uelewa wa mada husika
  • Ushirikishwaji wa wanfunzi katika mnbinuj husika.

​

4 of 65

Mbinu ya onesho mbinu yawwza kutumika kwa ufanisi kupitia aina hizi za onesho mbinu

  • Onesho halisi
  • Michoro
  • Video za kielimu
  • Mifano ya kimaumbile
  • Simulesheni za kompyuta na michezo ya kuigiza.

​

5 of 65

Onesho halisi�

  • Ni aina ya onesho mbinu ambalo linahusisha onesho la majaribio madogo madogo ambayo hufanyika darasani na wanafunzi wakamtazama mwalimu akiwa anafanya hatua kwa hatua kisha amwalimu huwaruhusu wanafunzi kuiga hatua kwa hatua kile alicho kuwa anakifanya mwalimu.
  • Katika eneo hili mwalimu anapaswa kuwepo darasani kuangalia kile ambacho wanafunzi wanakifanya na kutoa usaidizi mahali ambapo wanafunzi wanakwama.
  • Onesho halisi linaweza kuhusisha maonesho ya nadharia za kisayansi kama vile mabadiliko ya hali ya vitu, au michakato ya kikemikali. Mfano:kutumia maji baridi na ya motokuonesha jinsi joto linavyoongezeka nishati mwendo ya molekyuli.

​

6 of 65

Michoro�

  • Michoro inaweza kuwa onesho mbinu pale inapochorwa hatua kwa hatua mbele ya darasa kisha mwalimu kuwataka wanafunzi kufuatisha namna ya kuchora maichoro hiyo.
  • Michoro ikitumika vizuri huwasaidia wanafunzi kuona dhana mbalimbali za kisayansi. Mfano michoro ya mzunguko wa maji, mzunguko wa caboni, au seli za mimea na Wanyama.
  • Video za kielimu
  • Hizi nazo huwa sehemu za onesho mbinu kutokana na kwamba zinafafanua dhana ambazo kwa namna Fulani ni ngumu kueleweka kwa kutumia maneno pekee, wanafunzi wanaweza kuona, kusikia na kufuatisha kile walichoona hatua kwa hatua. Lakini pia video za kielimu hutoa mwonekano halisi wa mambo mbalimbali. Mfano video zinazoonesha jinsi mbegu zinavyoota.

​

7 of 65

  • Mifano ya kimaumbile
  • Inahusisha mambo yote yanayohusianisha mambo yanayojitokeza katika maumbile bila kuathiriwa na shughuli za kibinadamu. Mifano ni maumbile inayoweza kutumika ni kama vile mfumo wa jua, molekyuli za kemikali au mifumo ya kibailojiaa.
  • Simulesheni za kompyuta na michezo ya kuigiza.
  • Simulesheni za kompyuta ni aina ya onesho mbinu ambapo inatumika kuelezea dhan ambazo ni ngumu na tata kwa urahisi. Simulesheni zinaruhusu kufanya uhariri wa sauti, picha hata mandishi hivyo kurahisisha mahiri husika kueleweka kwa urahisi kwa wanafunzi.
  • Hii ni tofauti na video za kielimu, video hizi huwa haziruhusu kufanyiwa uhariri. Mifano michakato kama mabadiliko ya hali ya hewa,majaribio ya maabara au mizunguko ya kibailojia kama mzunguko wa seli n.k.
  • Simulesheni husaidia wanafunzi kuhusianisha nadharia ngumu na hali halisi huku wakijenga uelewa wa kina dhidi ya dhana ngumu.

8 of 65

mambo manne muhimu ya kuzingatiwa kabla ya kutumia mbinu ya oneshombinu.

  • Upatikanaji wa mahitaji yanayohitajika
  • Kiwango n/Uwezo wa wanafunzi
  • Idadi ya wanafunzi
  • Mahali pa kufanyia onesho mbinu
  • Tahadhari za kuchukuliwa wakati wa oneshombinu
  •  

​

9 of 65

Hatua za kufuata katika kutumia onesho mbinu.

  • Kuweka malengo ya kujifunza
  • Kuchagua na andaaa vifaa vya kutumia
  • Kufanya onesho mbele ya darasa hatua kwa hatua
  • Kuwaruhusu wanfunzi nao kufanya kwa vitendo kile ambacho mwalimu amefanya
  • Kutoa muda wa wanafunzi kuul;iza maswali
  • Kuwaruhusu wanafunzi kufanya majadiliano
  • Kufanya hitimisho

​

10 of 65

Umuhimu wa mbinu ya onesho mbinu.

  • Husaidia dhana ambazo ni ngumu au tata kueleweka kwa urahisi.
  • Inavuta usikivu kwa wanafunzi
  • Kuwezesha wanafunzi watumie milango mingi ya fahamu kuhusika katika ujifunzaji.
  • Huchochea ari ya ujifunzaji kwa wanafunzi
  • Kukuza uwezo wa kumbukumbu kwa muda mrefu.

​

11 of 65

Changamoto za onesho mbinu

  • Inagharimu muda katika uundaji
  • Inahusisha gharama kwa maana ya upatikanaji wa baadhi ya vifaa
  • Upungufu wa vifaa na rasilimali
  • Kutofautiana kwa mitindo ya kujifunza

​

12 of 65

Vigezo vinahitajika ili mbinu ya oneshombinu iweze kutumika kwa ufanisi katika somo la sayansi.

  • Maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuelewa mada namalengo husika.
  • Ushirikishwaji wa wanafunzi. Hii itachochea na kuhamasisha udadisi na ubunifu hasa pale wanafunzi wakiruhusiwa kufuatisha kile mwalimu amekitenda.
  • Kuandaa zana na vifaa vya kuwezesha hilo onesho mbinu
  • Wanafunzi wapatiwe muda wa kutosha ili wanafunzi waweze kujifunza kwa kina
  • Usimamizi mzuri wa darasa hasa pale wanafunzi wakiwa wanafuatisha onesho mbinu hiyo ili kutoa usaidizi pale inahitajika.

​

13 of 65

Maswali ya kuuliza wanafunzi kutoa maoni kuhusu ufanisi wa oneshombinu.�

  • Je ulipendezwa na onesho mbinu ? kwa nini. Swali hili litasaidia wanafunzi kufikiri vipengele vya onesho mbinu, muundo, mada, hata wahusika
  • Ni vipengele gani vya onesho mbinu vilikufanya ujiamini katika ujifunzaji?
  • Je kulikuwa n asehemu yoyote ya onesho ambayo hukuielewa vizuri? Ni ipi? Swali hili litaaidia kubaini eneo ambalo wanafunzi wanahitaji usaidizi Zaidi.
  • Ungependa kuona mabadiliko gani katika mbinu za uwasilishaji zinazotumiwa? Swali hili litasaidia wanafunzi kuttoa mapendekezo namna ambavyo mbinu hii inaweza kuboreshwa.
  • Je ungependa kujaribu aina nyingine za mbinu za uwasilishaji ? kama ndiyo ni zipi? Itasaidia kujua kama wanafunzi kuna njia tofauti katika uwasilishaji labda ni onesho halisi, video za kielimu, simulesheni za kompyuta au mifano ya maumbile
  • Ni vipi unaweza kutumia maarifa uliyoyapata kutoka kwenye onesho hili katika Maisha ya kila siku? Swali hili huwafanya wanafunzi wafikiri matumizi ya maarifa waliyopata jinsi yanavyoweza kuathiri Maisha yao
  • Je kuna jambo lolote ungependa kuongeza au kubadilisha kuhusu onesho hili? Swali hutoa fursa kwa wanfunzi kutoa maoni yao namna ya kuboresha ilionesho kuwa bora Zaidi kwa wakati mwingine.

​

14 of 65

Ufundishaji na ujifunzaji wa kutumia mbinu ya kisa mafunzo�

  • Ni mbinu ya ufundishaji inayotumia masimulizi au mifano halisi katika kuwasaidia wanafunzi kuelewa dhana inayowezeshwa ili wahusianishe na uzoefu wao wa Maisha.

Hatua za kufuata katika kutumia ,mbinu ya kisa mafunzo

  • Mwalimu achague au atengeneze kisa kinachohusiana na dhana ya kisayansi inayofundishwa. Kwa mfano kisa kinaweza kujumuisha hali ya ambapo jamii inakabiliana na tatizo la uchaguzi wa mazingira.
  • Wasilisha kisa kwa wanafunzi kwa njia ya maandishi video au mazungumzo
  • Shirikisha wanafunzi katika mijadala ya vikundi au darasa zima ambapo wanajadili matatizo yaliyotajwa kwenye kisa.

​

15 of 65

  • Baada ya majadiliano wanfunzi wanatakiwa kufanya maamuzi kuhusu suluhisho bora Zaidi la tatizo lililotajwa kwenye kisa.
  • Wanfunzi wahusishe dhana za kisyansi waliojifunza darasani na hali haliosi zinazotokeza katika kisa.
  • Toa fursa kwa wanafunzi kufanya tathimini ya matokeo ya maamuzi yao kwa kujiuliza maswali kama vile je suluhisho walilopendekeza linatekelezeka?au linaweza kutatua tatizo kwa ufanisi.

​

16 of 65

  • Umuhimu wa kutumia mbinu ya kisa mafunzo
  • Kuimarisha uelewa wa wanafunzi kwani wataelewa dhana ngumu kupitia mifano halisi kwa kutumia aau matukio yanayohusiana na mahiri wanayowezeshwa
  • Kuongeza ushirikiano wanafunzi wanaposhiriki majadiliano kuhusu kisa Fulani na kutaka kupata suluhisho la kisa hicho watabadilishana maoni na mitazamo tofauti, hali itakayowafanya wawe karibu Zaidi katika shughuli za kitaaluma.
  • Kukuza ujuzi wa fikra za juu kama vile uchambuzi tathmini na ubunifu. Wanfunzi wanapojadiliana kina pamoja na kuchambua kutafakari kwa matukio yaliyopo katika Fulani wanakua wadadisi na waweze kutoa maoni juu ya kupata suluhisho
  • Kuboresha ujuzi wa mawasiliano wanafunzi hujifunza jinsi ya kueleza mawazo na maoni yao kwa uwazi na kusikiliza kwa makini maoni ya wengine katika kukielewa kisa na namna watakavyo suluhisha changamoto zilizopo ndani ya kisa hicho
  • Kufanya somo kuwa rahisi na kuongeza ari ya kujifunza kwa wanafunzi
  • Kuwafanya wanafunzi kuwa na kumbukumbu ya muda mrefu, katika kile walichofundishwa.

​

17 of 65

Changamoto za kutumia mbinu za kisa mafunzo

  • Tofauti katika uelewa wa wanafunzi inaweza kupelekea mwalimu kupata changamoto ya kuunda masimulizi au mifano halisi inayoweza kueleweka kwa kila mwanafunzi.
  • Huhitaji uwepo wa rasimali vifaa vya kutosha katik akuandaa na kukamilisha utumiaji wa mbinu husika, mfano kalamu, karatasi, au vitu halisi.
  • Maabadiliko ya muktadha yanaweza kupelekea mazingira yasitoe mifano ya vitu halisi.
  • Mwalimu asipokuwa na uwezo mzuri wa kuandaa masimulizi inaweza kupeleka wanfunzi kushindwa kufikia lengo lillokusudiwa.

​

18 of 65

Jinsi ya kutumia mbinu ya majadiliano katika vikundi.

  • Maana ya majadiliano ni mbinu inayotumika katika ufundishaji na ujifunzaji ambayo inahusisha kitendo cha kupeana mawazo baina ya watu au pande mbili au Zaidi ili kufikia muafaka wa jambo Fulani.

Aina za majadiliano

  • Majadiliano ya mtu na mtu(majadiliano ya jozi)
  • Majadiliano ya kikundi
  • Majadiliano ya darasa
  • Majadiliano ya kitaaluma
  • ,majadiliano ya mtandaoni

19 of 65

Majadiliano katika vikundi

  • Aina hii ya majadiliano hufanywa na wanafunzi waliopo katika kikundi kilichoondaliwa na hupewa mada ya kujadili ambapo hushirikian na hubadilishana mawazo ili kuchambua dhana waliyopewa na kujenga uelewa wa kina kuhusu mada husika.

Aina hii ya majadiliano katika vikundi mambo yafuatayo ni lazima kufuatwa.

  • Hakikisha kwamba wanafunzi hawaundi makundi kufuata urafiki walionao
  • Uundaji wa vikundi lazima uzingatie ujumuishi
  • Uundaji wa makundi lazima uuzingatie urali wa jinsi

​

20 of 65

Mbinu zifuatazo unaweza kuzifuata katika uundaji wa vikundi

  • Panaga idadi ya wanafunzi unaotaka waunde kikundi kwa mfano kikundi cha wanafunzi watano
  • Ongoza wanafunzi kuhesabu namba moja hadi tano na kurudia mara kadhaa kwa wanafunzi wengine hadi kila mwanafunzi apate namba
  • Waelekezewanafunzi kukaa katika vikundi kulingana na namba walizohesabu.
  • Gawa majukum kwa kila kikundikwa kuzingatia mbinu ya majadiliano unayotaka kutumia.

​

21 of 65

Mambo ya kuzingatiwa katika mabinu hiii ya majadiliano katika vikundi

  • Kuwa na kiongozi na mwandishi kwa kila kundi
  • Kubainisha mud ana mada ya kujadiliwa
  • Kuruhusu majadiliano
  • Kusikiliza na kufuatilia kwa makini wakati wa majadiliano
  • Kuheshimu mawazo ya kila mshiriki anapotoa ufafanuzi pale inapohitajika
  • Kuruhusu wanafunzi wengi kuchangia majadiliano kadri iwezekanavyo
  • Kutoruhusu mwanafunzi mmoja kutawala majadiliano
  • Kuruhusu uwasilishaji wa vikundi ili vitoe majibu ya majadiliano
  • Kutoruhusu kikundi kurudia majibu yaliyokwisha tolewa na na kikundi kingine.

​

22 of 65

Ni wakati gani hasa majadiliano hasa majadiliano hutumika

  • Wakati unafanya marudio katika mada mbalimbali
  • Wakati unafundisha mada ambazo wanafunzi wana ufahamu wa mwanzo.mfano Elimu ya afya.
  • Baada ya wanfunzi kufanya jaribio la kisayansi au uchunguzi wa kitu Fulani.

​

23 of 65

Jukumu la mwalimu katika mbinu ya majadiliano

  1. Kutawala majadiliano kwa kuhakikisha hakuna kwanfunzi anayetawala majadiliano kuzidi wenzake
  2. Uliza maswali yenye changamoto tofautitofauti katika makundi mabalimbnali
  3. Kusisitiza wanafunzi wanapojadili kusikika kile wanachokisema
  4. Mwalimu ahakikishe nidhamu ya darasa inazingatiwa
  5. Mwalimu anapaswa kuhakikisha wanafunzi wanajadili kile wanachopaswa kujadili. Kwa maana nyingine wanapaswa kutotoka nje ya mada
  6. Mwalimu aandae ufupishao sahihi wa kile kilichokuwa kinadajadiliwa.

​

24 of 65

Vigezo vinavyotumika kupima ufanisi wa mbinu ya majadiliano katika vikundi

  • Kiwango cha ushirikiano miongoni mwao kusaidizana kufikia lengo husika
  • Kufikia lengo husika lililokuwa limepangwa kabla ya majadiliano
  • Ubora wa mawasiliano yanavyofanyikamiongoni mwao
  • Uwezo wa uwasilishaji. Pindi wakiwa wanawasil;isha kazi zao unaweza kujua kama wamefanya kwa ufanisi

​

25 of 65

Faida za kutumia mbinu ya majadiliano katika vikundi

  • Hukuza na kuendeleza stadi ya mawasiliano kwa wanfunzi
  • Hukuza ari ya kujiamini miongoni mwa wanfunzi hasa pale wakito majibu sahihi
  • Kukuza mtazamo wa kuheshimu mawazo yaw engine hasa pale wakiwa wnatoa mawazo yao kipindi cha majadiliano
  • Huchochea na kukuza fikra tunduizi
  • Mbinu hii huruhusu stadi ya ushirikiano kwa wanfunzi.

​

26 of 65

Changmoto ya mbinu ya majadiliano katika vikundi

  • Huhitaji muda wa kutosha ili kukamilisha mbinu hii
  • Huwa haifai kwa mada ambazo wanafunzi hawana uelewa wa awali au uzoef na hiyo mada
  • Inaweza kupelekea majadala katika mada ambazo hazihitajiki kwa muda huo
  • Wanfunzi wenye aibu kuzungumza mbele ya watu wengi wanaweza wasinufaike na mbinu hii
  • Wanfunzi wenye uelewa wa juu wanaweza kutawala mjadala.

​

27 of 65

Vigezo vya kupima ushiriki wa mwanafunzi katika mbinu ya majadiliano katika vikundi

  • Ushiriki halisi wa mwanafunzi(active participation)
  • Stadi za mawasiliano
  • Ushirikiano katika utatuzi wa matatizo
  • Uwezo wa kufikiri kimantiki
  • Matumizi ya lugha sahihi
  • Uwezo wa kufanya tathimini ya ndani ya kikundi.( peer assessment awareness)
  •  

​

28 of 65

Ufundishaji na ujifunzaji wa uchunguzi sahili wa kisayansi�

Uchunguzi ni mchakato unaotumia mbinu za kiutafiti ili kuboresha na kulete ufanisi katika mchakato wa ujifunzaji na ufundishaji.

Uchunguzi sahili wa kisayansi ni mchakato wa utafitii unaohusisha hatua za ukusanyaji wa data ,uchambuzi na kutoa hitimisho kuhusu maswali au tatizo linalochunguzwa.

Mambo ya kufikiriwa unapoandaa uchunguzi

  • Upatikanaji wa vifaa vyote vinavyohitajika
  • Kama uchunguzi utafanywa katika vikundi waza kuhusu ukubwa wa vikundi kuendana na ukubwa wa darasa.

​

29 of 65

Maandalizi kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi

  • Kusanya rasilimali zote zinazohitajika
  • Bainisha eneo ambapo uchunguzi huu utafanyika
  • Gawa wanfunzi katika vikundi vidogovidogo kama itahijika kufanya hivyo. Chagua na viongozi wa vikundi hivyo
  • Wanafunzi wafundishwe kwana nadgaria ya kile waanachoenda kukichunguza
  • Toa kazi ambayo sasa itawataka kufanya huo uchunguzi

​

30 of 65

Jukumu la mwalimu wakati wa uchunguzi

  • Kuwapatia wanafunzi mahitaji yote yanayohitajika katika uchunguzi wao.
  • Kutoa maelekezo yakutosheleza namna ambavyo jaribio hilo laweza kufanyika
  • Simamia mchakato wa uchunguzi kwa lengo la kuwatia moyo, kuwapa usaidizi na kusimamia nidhamu ili wafikie lengo husika
  • Fanya tathimini wakati wanaendelea na uchunguzi hadi hatua ya mwisho.

​

31 of 65

Hatua za kufuata katika kutumia mbinu hii ya uchunguzi wa sahili za kisayansi.�

Kubaini tattizo

  • Hatua hii inahusisha kubaini chanzo cha tatizo au jambo linalohitaji kupatiwa ufumbuzi wa kisayansi.

Kubuni dhanio au swali la utafiti

  • Dhanio ni majibu ya kubuni kuhusu tatizo lililobainishwa katika hatiua ya kwanza. Mara zote bunio halihusishi utafiti ili au kukusanya taarifa kuhusu jambo lillilobainishwa.hivyo bunio laweza kukubaliwa au kukataliwa mara baada ya hatua zingine za uchunguzi kukamilika. Bunio hukubalika endapo tu data zilizopatikana kuendana na bunio hilo. Kama hazijaendana bunio hukatalia
  • Swali la utafiti: ni swali linalobuniwa na mtafiti ili kupata majibu yanayoweza kuelezea tatizo lilobainika.

​

32 of 65

Kufanya jaribio

  • Hatua hii huhusisha ufanyika wa jaribio ambapo mtafiti au mchunguzi huandaa vifaa vyote vinavyo hitajika katika jaribi hili lakini pia huhusisha kupangilia vifaa hivyo. Katika sehemu hii mchunguzi anaweza kuandaa majaribi mawili ambapo jaribio moja hutambulika kama jaribio rejea(experiment control) hii hutegemea na jaribio linalofanywa.

Kukusanya data au taarifa.

  • Ukusanyaji wa data hufanyika sambamba na ufanyikaji wa jaribio wakati mtafiti au mchunguzi akiendeleana jaribio anapaswa kuandika au kurekodi kile kinachoonekana au kusika katika jaribio. Data inahitaji kurekodiwa kwa umakini ikijumuisha kuona, kusikia, kunusa, kugusa hata kuonja kama itahitajika. Katika hatua hii inapaswa kuwa makini san aili iweze kuchambuliwa na kutoa majibu sahihi ya kile kilichochunguzwa.

Kuchambua data.

  • Uchambuzi wa data hufanyika kwa kupanga data hizo katika utaratibu mzuri. Data hizi zilizopatika kutoka kwenye jaribio zinaweza kulinganishwa ili zitumike kubaini chanzo cha tatizo linalochunguzwa.

​

33 of 65

Kutafsri matokeo

  • Data zilizochambuliwa hutafsriwa na matokeo yake kuhifadhiwa. Majibu ya uchambuzi wa data yanaweza kutolewa kwa njia ya maelezo , chati , grafuu au jedwali ambayo husaidia kurahisisha kutafsri matokeo.

Hitimisho.

  • Katika hatua hii ndipo mchunguzi anaweza kuthibitisha(kukubali ) bunio au kukanusha( kulikataa) kwa kuhusianisha na mabunio na data za uchunguzi zilizopatikana baada ya jaribio kufanyika. Ikiwa dhanio litaendana na data za za jaribio basi bunio litathibitishwa na kama mabunio hayakubaliana na data za majaribio dhanio litakanushwa.

Kuandika taarifa

  • Baada ya uchunguzi kukamilika kwa kufuata hatua zote kwa usahihi hatua ya kuandika taarifa hufuata kwa kuandika mchakato wote ikijumuisha mambo yote yaliyofanyika kuanzia hatu aya kwanza hadi hatua ya hitimisho.

​

34 of 65

Umuhimu wa kutumia mbinu ya uchunguzi sahili wa kisayansi

  • Huongeza uelewa kwa wanfunzi
  • Humfanya mwanafunzi kujifunza kwa vitendo Zaidi
  • Humjengea mwanfunzi kumbukumbu ya muda mrefu
  • Hukuza stadi ya ushirikiani miongoni mwao hasa ikifanyika katika vikundi
  • Humjengea na kukuza stadi ya udadisi kwa mwanfunzi
  • Husaidia kuwatambua wanafunzi wenye uelewa wa chini na kuwasidia kwa wepesi
  • Hukuza ari ya kujifunza kwa wanfunzi
  •  

​

35 of 65

Changamoto za kutumia mbinu hii ya uchunguzi sahili wa kisayansi

  • Hutumia muda mrefu Zaidi
  • Ni ghari kutokan amuda mwingine humlazimu mwalimu kununua baadhi ya vifaa ili kufanikisha uchunguzi huo
  • Inamtaka sana mwalimu kuwepo hasa kipindi cha maandalizi, na kufanya usimamizi wakati uchunguzi unaendelea.
  • Baadhi ya kazi za uchunguzi huhitaji kuwa na maarifa ya kutosha ili kukamilisha uchunguzi kwa usahihi.

Tanbihi: uchunguzi sahili wa kisayansi unahusisha mbinu kama ziara ya mafunzo,majaribio ya maabara au simulesheni kwa kutumia kompyuta.

​

36 of 65

Jinsi ya kutumia mbinu ya kazimredi.

  • kazi mradi ni mbinu ya ufundishaji inayowahusisha wanafunzi katika kujifunza kwa kufanya kazi kwenye miradi kwa vitendo.
  • Mbinu hii huwataka wanafunzikujifunza kwa vitendo Zaidi kupitia miradi inayohusisha uchunguzi na utatuzi wa matatizo katika mazingira halisi badala ya kujifunza kwa nadharia tu.
  • Kwa ufupi mbinu ya kazi mradi inahusisha kazi za vitendo zinazofanyika nje ya darasa zikuhusisha miradi inayomtaka mwanafunzi kuchunguza na kutatua matatizo .

​

37 of 65

Mambo yafuatayo ni muhimu kuzingatiwa ili kufanikisha kazi mradi

  • Kuwaongoza wanfunzi kuchagua mada watakayofanyia kazimradi
  • Eleza nini unachotaka wanafunzi wajifunze kupitiia kazi mradi hiyo
  • Toa mwongozo kuhusu nini watahitaji kufanya ili kutimiza malengo hayo,kwa mfano wanfunzi kuelewa mchakato wa mabadiliko ya tabia nchi kukusanya na kuchakata data na kuwasilisha matokeo yake.
  • Ushirikiano mkubwa unatakiwa kati ya wanafunzi na mwalimu katika kuamua mad ana madhumuni ya kazi mradi hiyo
  • Gawa wanafunzi katika vikundi vidogo ili kutoa nafasi ya kushirikiana na kujifunza pamoja. Kwa mfano kila kikundi kinaweza kuwa na majukum tofauti kulingana na nguvu na vipaji vya wanakikundi

​

38 of 65

  • Panga jinsi kazi mradi itakavyotekelezwa kuanzia kukusanya taarifa hadi kuwasilisha matokeo. Toa mwongozo na msaada inapohitajika laikni ruhusu wanafunzi kuchukua jukumu kubwa katika kupanga na kutekeleza kazimradi.
  • Kuandaa nyenzo na zana za kufanya kazi maradi hiyo kama vile michoro , modeli , simu, kamera na daftari na kalamu
  • Kluwasaidia wanafunzi kutatua matatizo yanayoweza kutokea wa utekeleaji wa kazimradi
  • Kuwasidia wanafunzi kufuatilia na kutathimini mafanikio ya kazimradi kwa kuwapa ushauri na maelekezo ya kutosha
  • Kuwaongoza wanafunzi kuwasilisha matokeo ya kazi maradi kwa darasa zima walimu au hata kkwa jamii. Hii inaweza kufanyika kupitia wasilisho la mdomo ,maonesho au ripoti iliyoandikwa.
  • Pima uwezo wa wanafunzi kuelezea mchakato wao, matokeo yao na kujibu maswalikuhusu kazoi yao
  • Toa tathimini ya jinsi kila kikundi na mwanafunzi mmoja mmoja alivyotekeleza kazi mradi. Tathimini ushirikiano wao, ubora wa kazi zao na uwezo wao wa kutatua matatizo.

​

39 of 65

Maandalizi ya kazi mradi

  • Wanafunzi kugawiwa katika vikundi kuzingatia uwezo wao wa uelewaa. Mwanaunzi mwenye uwezo mkubwa awe kiongozi
  • Wanafunzi wapewe maelekezo ya kutosha kuhusu kile wanachopaswa kufanya, hakikisha kwamba kazi watakazo zipewa zinatosheleza na kuwafanya wote kushiriki ipasavyo.
  • Weka nyenzo za marejeleo zipatikana kwa wanafunzi wanapozihitaji.
  • Toa vifaa vya kazi pamoja na nyenzo zinzpohitajika.

​

40 of 65

Jukumu la mwalimu wakati wa kazimradi.

  • Kuwaongoza na kuwapa wanafunzi usaidizi wakiwa wanafanya kazimradi
  • Kufanya tathimini ya wanafunzi katika utendaji wa kazi yao
  • Kuwatia moyo na hamasa wanafunzi kwa kuonesha unavutiwa na kazi yao.
  • Kuwapa wanafunzi nyenzo wanazozihitaji
  • Kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanashiriki katika kazimradi husika

41 of 65

Ufanisi wa kazimradi

  • Kuweka malengo wazi na yanayoelewea ya kazimradi
  • Kugawa majukum kwa haki kulingana na uwezo wa mwanafunzi
  • Wanafunzi kufanya kazi kwa kushirikiana
  • Kutengeneza ratiba ya utekelezaji wa shughuli za mradi
  • Kufanya utafiti na ukusanyaji wa taarifa sahihi
  • Matumizi sahihi ya rasilimali kama vile vifaa, mud ana fedha.
  • Kufanya tathimini ya mara kwa mara.
  • Kuandaa na kuwasilisha ripoti bora inayovutia na inayoonesha uelewa wa kina .

​

42 of 65

Kazimradi inavyoweza kuhusianisha mwalichojifunza na Maisha ya mwanafunzi ya kila siku.

  • Kuwezesha ya maarifa kwa vitendo:Wanafunzi hutumia maarifa waliyojifunza kutatuaa matatizo halisi .
  • Kujenga stadi za Maisha: hujifunza kufanya kazi kwa ushirikiano,kupanga, kuchambua na kuwasiliana vizuri
  • Kukuza fikra hu una ubunifu:mbinu hii huwapa wanafunzi uhuru wa kuchunguza, kuuliza maswali na kuja suluhisho bunifu kwa matatizo ya jamii
  • Kuhusianisha mazingira ya mwanafunzi: miradi mingi huchaguliwa kutoka katika mazingira anayotoka mwanafunzi hivyo humwezesha mwanafunzi kujona uhusiano wa moja kwa moja
  • Kuwajengea uwajibikaji:kazimradi huwataka wanafunzi kuwa na majukum maalum hivyo katika utekelezaji wa majukum hayo hujikuta wanajifunza kuwajibika n akutimiza majukum.
  • Kuwezesha ujifunzaji wa kina na wakudumu;maarifa yanayopatikan akwa njia ya kufanya hubaki kwa muda mrefu hivyo kuendelea kutumika katika Maisha yao ya kila siku.

​

43 of 65

Vigezo muhimu vinavyotumika kutathimini kazimradi

  • Ushiriki wa mwanafunzi:anagalia kama mwanafunzi alichangia kikamilifu katika kazimradi
  • Ujuzi wa vitendo:angalia uwezo wa mwanfunzi kutumia vifaa, kufuata taaratibu za kazi na kutekeleza majukum yake.
  • Ushirikiano katika kikundi
  • Uwasilishaji wa matokeo ya kazimradi:hii inahusisha matumizi mazuri ya lugha katik auwsilishaji na uelewa wa kile anachowasilisha
  • Uzinagatiaji wa muda na maelekezo
  • Ubunifu na utafiti: angalia kama mwanafunzi alionesha fikra mpya kuuliza maswaliya kina au kubuni njia bora ya namna ya kutekeleza jukuim hilo.

​

44 of 65

Namna ya kushughulikia changamoto zinazojitokeza wakati wa kutekeleza kazimradi�

s/n

Changamoto

Namna ya kushughulikia changamoto11

1

Ukosefu wa ushirikiano miongoni mwa wanafunzi

-kila mwanafunzi kupewa jukum lake ili awajibike

-fanya ufuatiliaji wa karibu na mahojiano ya kikundi ili kubaini nani hawajibiki

2

Upungufu wa rasilimali(vifaa, muda fedha)

tumia vifaa vinavyopatikan akirahisi

-pangilia kazimradi kulingana na muda uliopo

Shirikisha wazazi na jamii kwa msaada wa vifaa

3

Kukosekana kwa mwongozo wakutosha.

kutoa mwongozo wa kutosha mara kwa mara

-toa msaada wa kitaaluma na kiufundi wakati wa utekelezaji

4

Wanafunzi kukosa ujuzi wa kupanga au kuchunguza

fanya mafunzo ya awali namna ya kufanya kazi mradi

-toa mifano ya kazimradi iliyofanikiwa ili kuwapa mwelekeo

5

Muda kutotosha kukamilisha mradi

-pangilia mradi kwa awamu ndogo ndogo zenye malengo madogo

-hakikisha kuna ufuatiliaji wa kila hatua na kutoa motisha kwa wanaokamilisha kwa muda.

6

Kukosekana kwa uadilifu wa kazi(kutegemea wengine)

himiza maadili ya uaminifu kwa kuwajengea wanafunzi wa thamani ya kazi yao binafsi

-fanya mahojiano ya mdomo kwa wanafunzi kueleza walichofanya

45 of 65

Umuhimu au faida wa kazimradi

  • Hufanya ujifunzaji kuwa ni jambo la kuvutia
  • Humpa mwanafunzi kutumia ubunifu wake mwenyewe
  • Humfanya mwanafunzi kujifunza yeye mwenyewe
  • Huwasidia wanafunzi kukuza mitazamo mbalimbali ya kisayansi kama vile uongozi,ushirikiano na uwezo wa kujiamin
  • Huchangia upatikanaji wa stadi mbalimbali za kisayansi kama uchunguzi, upimaji na kurekodi(kuhifadhi)

​

46 of 65

Jinsi ya kutumia ya mbinu ya majaribio katika ufundishaji na ujifunzaji�

  • Mbinu hii huwataka wanafunzi kupata maarifa kwa kufanya uchunguzi wa jambo Fulani ikihusisha kutatua tatizo pamoja na mbinu za ugunduzi wa jambo.
  • Mambo ya kuzingatiwa katika utumiaji wa mbinu hii ya majaribio
  • Kuweka malengo uya wazi namakusudi ya majaribio. Hii husaidia katika kubaini nini kinachotakiwa kupimwa au kuchunguzwa
  • Kufanya tafakuri ya awali mna kutengeneza dhanio linalojibu maswali au linaloeleza uhusiano wa sababu na athari
  • Kutengeneza mpango wa kina wa jinsi majaribio uyatavyoendeshwa ikiwa ni pamoja na muundo wa majaribio njia za ukusanyaji wa data na mbinu za uchunguzi

​

47 of 65

  • Kuhakikisha usalama na ustawi wa wanafunzi unazingatiwa
  • Kufanya majaribio kadhaa ili kuhakikisha kwamba matokeo kwamba matokeo yanakuwa thabiti
  • Kuhakikisha data inayokusanywa ni sahihi, kamili na inarekodiwa kwa usahihi
  • Kutengeneza tahimini na uchambuzi wa matokeo kwa kutumia mbinu sahihi za takwimu na uchambuzi ili kujua kam adhanio imethibitishwa au kupingwa.
  • Tayarisha ripoti kamili ya majaribio inayojumuisha maelezo ya jinsi majaribio yaliyofanywa, matokeo yaliyopatikana na tafsri ya matokeo

​

48 of 65

  • Maandalizi ya mbinu ya majaribio
  • Kuandaa nyenzo na vifaaa vya majaribio vinavyohitajika
  • Panga mchakato wa jaribio ukiwemo udhibiti wa jaribio kama inahitajika
  • Panga wanafunzi katika vikundi vidogo kama inahitajika chagua na kiongozi wa kikundi hicho.

​

49 of 65

Jukumu la mwalimu katika mbinu hii ya majaribio

  • Kuwapatia wanfunzi vifaa vyo vinavyohitajika katika jaribio husika
  • Kuhakikisha unawapa wanafunzi maelekezo ya kina kuhusian na namna ambavyo jaribio linaweza kufanyika hatua kwa hatua
  • Wape angalizo kuhusiana na ajari ambazo zinzweza kujitokeza wakati wanfanya uchunguzi katika jaribio lao
  • Kuwapa usaidizi wanafunzi wa namna ya kuchukua au kurekodi data wakati wa uchunguzi ukiendelea
  • Wasimamie wanafunzi ili kudhibiti nidhamu zao na kuwapa usaidizi pale inapohitajika
  • Fanya tathimini namna ambavyo wanafunzi wanabeba vifaa vya majaribio

​

50 of 65

Ni muhimu kuweka kikomo cha idadi ya wanfunzikatika ufanyikaji wa majaribio. Kwa sababu zifuatazo:-

  • Kuimarisha usalama wa wanafunzi wakti jaribio linafanyika
  • Kuhakikisha ushiriki wa kila mwanfunzi katika jaribio wanalofanya
  • Kuwezesha usimamizi bora, usaidizi na ufuatiliaji wakati wakifany ajaribio
  • Matumizi bora ya vifaa na nyenzo
  • Kuwezesha kufanya tathimini iliyo bora zaidi

​

51 of 65

Umuhimu wa kutumia mbinu ya majaribio katika mchakato wa ufundishsji na ujifunzaji

  • Huwafanya wanafunzi kuwana kumbukumbu ya muda mrefu kuhusu kile walichojifunza
  • Wanafunzi huwa wanajenga kuamini maarifa waliyoyapat katika jaribio husika
  • Wanafunzi hujifunza kujifunza wao wenyewe bila kutegemea usaidizi
  • Huchochea upatikanaji wa ujuzi wa kisayansi mfano ubebaji wa vifaa vya majaribio
  • Mbinu hii huchochea na kuendeleza mitazamo chanya ya kisayansi kama vile udadisi na ushirikiano.
  • Mbinu hii huhusisha ujifunzaji wa kutumia milamngo mingi ya fahamu

​

52 of 65

Changamota ambazo zinzweza kujitokeza katika utumiaji wa mbinu ya majaribio

  • Mbinu hii hutumia muda mwingi sana katika kukikamilisha
  • Mbinu hii inaweza isitumike kwa baadhi ya mada mfano mzunguko wa jua
  • Mbinu hii muda mwingine huwa ghari sana hasa ufagraguzi usipotumika. Kwa sababu baadhi ya vifaa huwa ghari sana.
  • Inaweza istumike vyema kwa baadhi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum. Mfano wasioona

​

53 of 65

Matumizi ya kutumia mbinu ya kualika mgeni

  • Mbinu ya kualika mgeni huwa hasa katika muktadha wa majaribio, mikutano, au matukio ya kitaaluma. Hivyo mbinu hii ya kualika mgeni inatumika kuleta mtazamo wa ziada , ujuzi maalum au uzoefu wan je ili kuongeza thamani ya shughuli.

​

54 of 65

Mambo ya kuzingatiwa katika kutumia mbinu ya kualika mgeni.

  • Kubainisha malengo ya kumualika mgeni
  • Kuchagua mgeni ambaye ana ujuzi, uzoefu na matazamo utakaosaidia wanafunzi kujenga umahiri uliokusudiwa
  • Kuwsiliana na mgeni mapema na kumpa taarifa kuhusu ratiba, mud ana malengo ya mada husika
  • Kufanya makubaliano ya wazi kuhuisu majukum ya, muda wa uwasilishaji na aina ya uwasilishaji unaohitajika
  • Kuandaa eneo na vifaa ambavyo mgeni atafanyia uwasilishaji
  • Kutayarisha mwongozo au nyaraka muhimu kwa mgeni kabla ya shughuli ili awe na ufahamu wa kina kuhusu kile kinachohitajika
  • Kutathimini mchango wa mgeni jinsi ulivyosaidia kufikia malengo ya mada au majaribio husika.

​

55 of 65

Umuhimu wa mbinu ya kualika mgeni

  • Husaidia kujenga ushirikiano baina ya mwalimu , mgeni na wanfunzi
  • Huchochea ari ya ujifunzaji kwa wanfunzi
  • Hutoa mtazamo mpya kwa wanafunzi pale ambapo mgeni maarifa aliyoyawasilisha yatakuwa yameeleweka.
  • Huijenga kumbukumbu ya muda mrefu kwa wanfunzi

​

56 of 65

Changamoto ambazo zinaweza kujitokeza katika mbinu ya kualika mgeni

  • Huhtaji wa kutosha katika kufanya maadalizi ya kumwalika mgeni
  • Ushirikishwaji wa wanafunzi unaweza kuwa mdogo endapo mgeni aliye alikwa atakuwa hana ujuzi wa kutosha katika uwasilishaji
  • Inaweza kupelekea upotoshaji hasa hasa pale mgeni atakuwa han amaarifa ya kutosha

​

57 of 65

Ufundishaji na ujifunzaji wa sayansi katika kubwa�

Darasa kubwa ni lile daras lenye idadi kubwa ya wanafunzi Zaidi ya wanafunzi 45 kwa mwalimu mmoja katika darasa.

  • Idadii ya wanfunzi kuwa kubwa imechangiwa na mambo mengi mojawapo ni
  • Ongezo la usajili wa shule za msingi na sekondari, shule hizi zimekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi ikilinganishwa na uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi

​

  • Sera ya “Elimu bure kwa watanzania wote” hasa katika elimu msingi hii imepelekea wanafunzi wengi kuandikishwa shule za msingi

​

58 of 65

  • Ongezo la watu katika maeneo mengi nchini ukilinganisha na shule za msingi zilizokuwepo toka miaka mingi
  • Mwitikio chanya wa wazazi dhidi ya Elimu.watu wengi wabadilika n akuona kuwa shule ni kitu cha lazima katika kipindi hiki.
  • Kutokana na wingi wa wanafunzi mashuleni umepelekea ufundishaj kufanyika katika ukumbi mdogo au mkubwa ambapo wanafunzi wengi huangia katika maeneo hayo kwa wakati mmoja.
  • Hivyo sasa matumizi ya mbinu sahihi na mipango mizuri lazima kuzingatiiwa katika ufundishaji wa darasa kubwa ili kufikia lengo husika.

​

59 of 65

  • Mwalimu anapokuwa anafundisha darsa kubwa anashauriwa kuwa mnyumbufu katika mbinu zake za ufundishaji ili kuendana na mazingira ya darasa halisi.
  • Namna ya kufundisha katika darasa kubwa
  • Mwalimu anapaswa kuandaa mpango makini wasomo unaozingatia malengo mahsusi na shughuli zinazohusisha wanafunzi wengi kwa kutumia mbinu mbalimbali kama zifuatazo:-
  • Vikundi vidogo vidogo: vikundi hivi view na watu kati ya 4-5 na mwalimu una jukukum la kuhakikisha kwamba kikundi hicho kina kiongozi na kila mwanakikundi anashiriki ipasavyo.

​

60 of 65

  • Matumizi ya teknolojia: mwalimu unatika kutumia video za elimu ,simulesheni za kiasayansi. Lakini pia vifaa saidizi kama vile spika, projrkta,luninga kubwa(big screen) maiki n.k vifaa hivi hufanya somo livutie lakini pia vifaa hivi vitasaidie kufuika wanafunzi
  • ufundishaji n aujifunzaji. Hii husaidia sana usimamizi wa darsa pia hutoa fursa kubwa ya kupata maoni tofauti , mitindo tofauti ya ufundishsji .
  • Kazi za ziada: mfano miradi ya vitendo,kazi za nyumbani,na uchunguzi.huhusisha wanafunzi wengi bila kujali mitindo yao mingi ya ujifunzaji.
  • Ufundishaji wa pamoja(team teaching): hii huhusisha walimu wawili au Zaidi kushirikian akatika

​

61 of 65

Namna ya kushughulikia utofauti wa viwango vya uelewa kwa wanafunzi katika darasa kubwa.�

  • Kuweka vikundi vya mchanganyiko: wanafunzi wenye uelewa tofauti wanaweza kufundishana kaupitia kazi za vikundi.
  • Kutumia mbinu mchanganyiko katika ufundishaji: unaweza kutumia mihadhara,majadiliano ya vikundi, vibonzo,michezo ya kielimu maswali na majibu ili kukudhi mitindo mbalimbali ya ujifunzaji wa wanafunzi
  • Kutoa kazi za viwango tofauti:tayarisha kazi zenye viwango tofauti vya ugumu ili kila mwanfunzi apate changamoto kutokana na kiwango chake cha uelewa.
  • Matumizi mazuri ya teknolojia:tumia vifaa ya kiteknolojia kama vile simu, kompyuta, projekta video za kielimu na maabara pepe. Hiui itaaidia kila mmwanfunza kupata uwezo wa kujifunza katika kona yake ya ujifunzaji
  • Kutoa msaada wa ziada : weka muda wako wa ziada nje ya muda wa kawaida kwa ajili ya wanafunzi wanaohitaji usaidizi
  • Kuongeza ushirikiano wa mwanafunzi mmoj mmoja: zungumza na mwanafunzi mmoja mmoja au kwa kikundi ili kuelewa hasa chanagamoto inayomsibu mwanafunzi
  • Kufanya tathumini za mara kwa mara:wapatie wanafunzi majaribio mafupi ya mara kwa mara ili kubaini mahitaji ya ujifunzaji ya wanafunzi wako.

​

62 of 65

  • Kazi kwa vikundi vidogo: kila kikundi kifanye jaribio au sehemu ya jaribio na kisha kiwasilishe. Hii mbinu inaweza Kupunguza msongamano wa vifaa na kuongesza ushirikiano
  • Tumia jaribio la kuonesha( demonstration):inaweza kutumika pale vifaa vi vichahcge au pale kama jaribio ni hatari
  • Tumia teknolojia hasa video za kielimu: amabapo zinaweza kutumika kuonesha majaribio ikiwa hakuna vifaa vya kutosha.
  • Tumia maabara pepe(virtual lab:hizi ni maabara za kielectroniki ambazo zitasaidia wanafunzi kufany ajaribio hata wakiwa wengi n ahata kama vifaa havitoshelezi.

​

63 of 65

Hatua za kuzingatiwa kuhakikisha usalama wa ufanyikaji wa majaribio katika darasa kubwa

  • Kutoa maelekezo ya usalama kabla ya jaribio
  • Kuhakikisha vifaa vyote vipo katika hali ya usalama
  • Kuwagawa wanafunzi katika vikundi vidogo
  • Kuhakikisha uwepo wa vifaa vya dharura.
  • Kuzuia ulaji au unywaji katika maabara
  • Kuhakikisha kuna usimamizi wa karibu wa mwalimu muda wote wa majaribio.

​

64 of 65

Vigezo vitumikavyo kutathimini majaribio yanayofanywa na wanafunzi katika darasa kubwa.

  • Ufuataji wa maelekezo: kuangalia kama mwanfunzi alifuiata hatua zote za jaribio husika kam ailivyoelekezwa.
  • Matumizi sahihi na nyenzo: kuanagalia kama mwanfunzi alitumia vifaa na kemikali vile ipasavyo
  • Usalama wakati wa jaribio; hata utaangal;iakam amwanfunzialieopuka vitendo vyote vya hatari wakati anendelea na jaribio
  • Ushirikiano katika kazi ya kikundi;
  • Uwezo wa kuchambuana na kutafri matokeo:kuangalia kama mwanafunzi ana uwezo wa kueleza matokeo kwenye jaribio na kueleza uhusaino kati ya hatua na matokeoa yaliyotokea.
  • Uwasilishaji wa matokeo: uwezo wa mwanfunzi kuandika taarifa ya jaribio husika
  • Ubunifu na uchunguzi wa kina:utangalia kuona kama mwanfunzi alionesha udadisi, kuuliza maswali ya ziada au kupendekeza mbinu bora Zaidi.

​

65 of 65