1 of 11

UCHOPEKAJI WA MASWALA MTAMBUKA KATIKA SOMO LA SAYANSI�

MBINU ZA UCHOPEKAJI MASUALA MTAMBUKA KATIKA UJIFUNZAJI NA UFUNDISHAJI

2 of 11

Utangulizi �

  • Masuala mtambuka ni mojawapo ya mambo ambayo yamehusishwa katika mtaala wa Elimumsingi wa mwaka 2023 ambao umetokana na Sera ya Elimu ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023.

3 of 11

Masuala mtambuka�

  • Maana ya masuala mtambuka
  • Ni mambo ambayo yanaibuka kwenye jamii ambayo yanaathiri maendeleo ya jamii kwa namna moja ama nyingine.
  • Mambo hayo yanaweza yakaibuka na kuendelea kwa muda mfupi na mengine yanaweza kuibuka na kubaki katika jamii kwa muda mrefu.
  • Mfano ugonjwa wa UKIMWI, masuala ya Jinsia, utumiaji wa dawa za kulevya, utunzaji wa mazingira na magonjwa ya mlipuko kama Covid 19.

​

4 of 11

Uchopekaji

  • Uchopekaji wa masuala mtambuka ni mbinu ya kuunganisha na kuingiza mada mbalimbali zinazovuka mipaka ya somo moja ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata maarifa na stadi za maisha.

​

  • Uchopekaji ni kitendo cha kuhusisha ufundishaji na ujifunzaji wa masuala mtambuka wakati wa kufundisha na kujifunza wa shughuli mahususi zilizopo kwenye muhtasari wa masomo.

​

5 of 11

Njia za kuchopeka masuala mtambuka�

  • Kuna njia mbalimbali ambazo mwalimu anaweza kuzitumia katika kuchopeka masula mtambuka wakati wa ufundishaji na ujifunzaji Mfano wa njia hizo ni pamoja na;
  • Mbinu za kufundishia na kujifunzia: Mwalimu anaweza kuchopeka masuala mtambuka kupitia mbinu mbalimbai ambazo atazitumia wakati wa ufundishaji na ujifunzaji.
  • Mfano mwalimu anaweza kuchopeka suala la ujumuishi kupitia mbinu ya majadiliano katika vikundi kwa kutengeneza makundi yenye watoto wenye mahitaji mbalimali kwa pamoja.

​

6 of 11

Njia za kuchopeka masuala mtambuka�

  • Zana za kufundishia na kujifunzia: Mwalimu anaweza kuchopeka masuala mtambuka kwa kutumia zana anazoziandaa kwa ajili ya kufundishia.
  • Mfano anaweza kuandaa picha au michoro ambayo kupitia michoro hiyo wanafunzi wanaweza kujifunza suala mtabuka fulani. Mfano suala la jinsia linaweza likachopekwa kwenye picha inayoonesha watoto wa kike wakiendesha mitambo kiwandani na watoto wa kiume wakiandaa chakula jikoni.

​

7 of 11

Njia za kuchopeka masuala mtambuka�

  • Shughuli au vitendo vinavyofanyika darasani: Mwalimu anaweza kuchopeka masuala mtambuka kupitia shughuli mbalimbali atakazo zifanya darasani.
  • Mfano wakati wa kuchagua watoto kujibu maswali au kupita mbele ya darasa kufanya matendo mbalimbali, hapa walimu wanaweza kuchopeka ujumuishi au jinsia.

​

8 of 11

Njia za kuchopeka masuala mtambuka�

  • Shughuli za nje ya darasa: Mwalimu anaweza kuchopeka masuala mtambuka kupitia shughuli mbalimbali zinazoweza kufanyika nje ya darasa.
  • Mfano mwalimu anaweza kuchopeka suala la ulinzi na usalama barabarani wakati wa kuagana na watoto kwenda nyumbani.

​

9 of 11

Kazi ya kufanya 1�

1. Andaa somo kuhusu mada ya magonjwa kwa darasa la nne na onesha jinsi utakavyotumia masuala mtambuka katika ufundishaji na ujifunzaji

2. Tumia uchunguzi wa kisayansi kuonesha athari za uchafuzi wa mazingira na andika ripoti kuhusu athari hizo kwa jamii inayokuzunguka.

​

10 of 11

Zoezi 1�

  1. Kwa kutumia oneshombinu katika vikundi vya watu wane, jadili jinsi uchopekaji wa masuala mtambuka unavyoweza kufanyika katika ufundishaji wa majaribio sahili ya kisayansi.

​

2. Fafanua jinsi uchopekaji wa mabadiliko ya hali ya hewa unavyoweza kufanyika katika uchunguzi wa mchakato wa fotosinthesisi

​

3. Eleza jinsi unavyoweza kuchopeka afya ya jamii, kama vile magonjwa ya mlipuko na jinsi sayansi inavyosaidia kutatua matatizo hayo ili yasitokee tena.

​

11 of 11