Sign in to Google to save your progress. Learn more

FOMU YA  MAONI YA WADAU KATIKA  MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO KUHUSU MKAKATI  WA USHIRIKISHWAJI  WA VIJANA KATIKA KILIMO (NSYEA 2026/27–2030/31)

FOMU YA  MAONI YA WADAU KATIKA  MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO KUHUSU MKAKATI  WA USHIRIKISHWAJI  WA VIJANA KATIKA KILIMO (NSYEA 2026/27–2030/31)


Wizara ya Kilimo inaandaa Mkakati wa Kitaifa wa Ushirikishwaji wa Vijana katika Kilimo (NSYEA) 2026/27–2030/31 kwa lengo la kuongeza ushiriki wa vijana katika shughuli za kilimo na biashara za kilimo, kuongeza tija na kipato, kuimarisha upatikanaji wa masoko, teknolojia, mitaji na huduma muhimu, pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kujihusisha kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa mazao.

Fomu hii inalenga kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa mazao, wakiwemo wakulima, vikundi na vyama vya ushirika, wazalishaji wa pembejeo, wafanyabiashara, wakusanyaji wa mazao, wasindikaji, wanunuzi wa mazao, wasafirishaji, taasisi za fedha, watoa huduma za teknolojia, sekta binafsi, taasisi za utafiti na mafunzo, Serikali na washirika wa maendeleo.

Maoni yako yatasaidia kuboresha Mkakati na kuhakikisha kuwa Maeneo ya mkakati na afua zilizopangwa zinazingatia changamoto, fursa na mahitaji halisi ya vijana katika mnyororo wa thamani wa mazao.

RASMU YA MKAKATI HUU INAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA WIZARA YA KILIMO

1. Jina la Mtoa Maoni

*
2. Jina la Taasisi/Kampuni/Kikundi *
3.  Aina ya taasisi: *
4. Mkoa *
5 . Halmashauri ya Wilaya *
6. Kata *
7. Ni hatua gani zinapaswa kuchukuliwa ili kuongeza ushiriki wa vijana katika uzalishaji wa mazao? *
SO1: Kuboresha tija, uzalishaji na kipato cha vijana katika kilimo

8. Ni huduma zipi muhimu zaidi vijana wanahitaji ili kuongeza tija na kipato?

*
9.  Una mapendekezo gani kuhusu SO1? *
10.  Ni hatua gani zinaweza kusaidia kuwaunganisha vijana na masoko yenye uhakika? *
SO2: Kuimarisha ushiriki wa vijana katika masoko na kuongeza thamani ya mazao
11.Ni fursa zipi za kuongeza thamani ya mazao unaziona zinafaa kwa vijana? *
12. Sekta binafsi inaweza kuchangia kwa namna gani katika kuwawezesha vijana kupata masoko? *
13. Una mapendekezo gani kuhusu SO2? *
14. Ni vikwazo gani vinazuia vijana kutumia teknolojia hizi? *

SO3: Kuharakisha matumizi ya teknolojia zinazoongeza tija na kuimarisha uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

15. Ni huduma zipi zinapaswa kuimarishwa ili kuongeza matumizi ya teknolojia na ubunifu? *
16.Unaona vituo vya ubunifu na teknolojia vinaweza kusaidia vijana kwa namna gani? *
17. Una mapendekezo gani kuhusu SO3? *
18. Ni changamoto zipi za uratibu kati ya wadau zinazoathiri ushiriki wa vijana katika mnyororo wa thamani? *
SO4: Kuimarisha mazingira wezeshi kwa ushiriki wa vijana katika kilimo
19.Una mapendekezo gani kuhusu SO4? *
20.Toa maoni katika Afua 15 zinazopendekezwa katika mkakati huu, nini kinatakiwa kuongezwa au kuboreshwa ili mkakati huu uweze kutekelezeka *
21. Kwa mtazamo wako, afua zilizopendekezwa zinaendana kwa kiasi gani na changamoto halisi za vijana katika mnyororo wa thamani wa mazao? *
22. Ni mabadiliko gani ungependekeza yafanywe katika Mkakati kabla ya kukamilishwa? *
23.Toa maoni ya ujumla katika mkakati huu *

ASANTE KWA KUSHIRIKI

Maoni yako ni muhimu katika kuandaa Mkakati unaozingatia mahitaji halisi ya vijana na wadau wa mnyororo wa thamani wa mazao.

Submit
Clear form
Never submit passwords through Google Forms.
This content is neither created nor endorsed by Google. - Terms of Service - Privacy Policy

Does this form look suspicious? Report