Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania inafanya mapitio ya Sheria ya Bima za Vyombo vya Moto, Sura ya 169 kwa lengo la kuiboresha ili iendane na mahitaji ya sasa ya sekta ndogo ya Bima. Sheria hii ni ya muda mrefu na utekelezaji wake umeonekana kuwa na changamoto. Sheria hii ilitungwa mwaka 1945 na kuanza kutumika mwaka 1946, ikiwa na lengo la kuweka masharti ya bima dhidi ya majanga yanayotokana na matumizi ya Vyombo vya Moto.
Ukiwa mdau muhimu wa Bima hapa nchini, Tume inakuomba kujaza dodoso hili kwa kutoa maoni yako kuhusu mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Bima za Vyombo vya Moto, Sura ya 169. Lengo la maboresho hayo ya Sheria ni kulinda maslahi ya wananchi, wamiliki wa vyombo vya moto/wakatabima, makampuni ya bima na wadau wengine.
Tunatanguliza shukran kwa kushiriki kutoa maoni yako kwa sababu ni muhimu katika kuboresha Sheria ya Bima ya Vyombo vya Moto, Sura ya 169.