MADA
YA PILI: MATUMIZI SAHIHI YA DAWA
Utangulizi
Kufanikishwa kwa tiba kutawezekana pale tu
mtoa dawa atakapoweza kutoa maelezo
ya matumizi sahihi ya dawa.
Matumizi ya Dawa
a)
Maana
ya matumizi sahihi ya dawa
Matumizi sahihi ya dawa hujumuisha mgonjwa
kupokea dawa sahihi kulingana na mahitaji yake ya kiafya, katika dozi sahihi,
muda sahihi wa matibabu.
b)
Matumizi
ya dawa yasiyo sahihi
Matumizi yasiyo sahihi ya dawa hujumuisha; Kutumia
dozi isiyo sahihi, kushindwa kumaliza kozi, kutumia dawa isiyo sahihi katika
kutibu ugonjwa, kutumia dawa kwa njia isiyo sahihi, kununua na kutumia dawa
kiholela bila kufanyiwa uchunguzi, kutumia dawa yenye viwango vya chini vya
ubora, kutumia dawa ambayo ni ghali bila sababu ya msingi, kutumia dawa zinazoingiliana
kiutendaji kwa pamoja mfano tetracycline na magnesium trisilicate, kutumia
viuavijasumu (antibiotics) kutibu magonjwa yanayotokana na virusi (viral
infections), kutumia dawa na pombe, kutumia dawa zisizoruhusiwa wakati wa
ujauzito mfano albendazole, doxycycline, phenytoin n.k
c)
Faida
za matumizi sahihi ya dawa
Kuboresha
afya ya mtumiaji wa dawa, kutimiza lengo sahihi la matumizi ya dawa husika, kupunguza
uwezekano wa kujenga usugu wa vimelea vya magonjwa, kupunguza madhara/maudhi ya
dawa, kupunguza gharama zisizo za lazima kwa mgonjwa na Serikali, kupunguza
uwezekano wa kupata magonjwa yatokanayo na utumiaji sugu wa dawa, jamii kuwa na
imani na dawa pamoja na mifumo ya kutolea huduma za afya .
d)
Sababu
zinazochangia matumizi yasiyo sahihi ya dawa
Kutogundua ugonjwa, uandikaji wa dawa usio
sahihi, utoaji wa dawa usio sahihi, mgonjwa kushindwa kumudu gharama ya dawa, mgonjwa
kutotumia dawa kwa usahihi, mgonjwa kujiamulia matumizi ya dawa bila kupata
ushauri wa Mtaalamu wa Afya.
e)
Mtoa
dawa anaweza kuchangia matumizi yasiyo sahihi ya dawa kama atafanya
yafuatayo:
·
Kushindwa kuelewa cheti cha mganga na kuacha
kuwasiliana naye ili kupata ufafanuzi,
·
kutoa dawa isiyo sahihi,
·
kushindwa kukokotoa au kutoa kiasi sahihi cha
dawa,
·
kuandika lebo kwa makosa au isiyosomeka
vizuri,
·
kutoa maelekezo yasiyojitosheleza kuhusu matumizi
ya dawa,
·
kushindwa kuhakikisha kuwa mgonjwa ameelewa
maelekezo ya matumizi ya dawa,
·
kutoa dawa au maelezo ya dawa bila kuzingatia
imani,
·
mazingira au mila za mgonjwa,
·
kushindwa kuhimili shinikizo la mgonjwa la
kutaka kuuziwa dawa ambayo kimsingi haiitajiki,
·
kutoa dawa kwa tamaa ya fedha bila kuzingatia
ubora wa huduma,
·
mgonjwa kushindwa kumudu gharama ya Dawa.
Kumekuwa na tabia/kasumba kwenye jamii kwa
baadhi ya watu kujiamulia kutumia dawa bila kumuona mtaalamu wa afya, hii
inaweza kusababishwa na mambo yafuatayo:-
·
Kujitibu kupitia kwenye mitandao (self treatment),
·
kufuata ushauri wa mtu ambaye sio mtaalamu wa
dawa,
·
matumizi ya dawa zilizobaki ambazo zilikuwa
za mtu mwingine au kuhifadhi dawa kwa matumizi ya baadae,
·
mgonjwa kushindwa kumudu gharama za kumuona
mtaalamu wa Afya,
f)
Athari
zitokanazo na matumizi yasiyo sahihi ya dawa
·
Mgonjwa hatapata tiba sahihi na hivyo
kuendelea kuugua au wakati mwingine kupelekea kifo ,
·
uwezekano wa kupata madhara ya dawa,
·
kuongezeka kwa usugu wa vimelea hii hutokea
zaidi kwa dawa aina ya viuavijasumu (antibiotics) na dawa za malaria,
·
kupoteza fedha nyingi katika matibabu na mgonjwa
kutegemea zaidi dawa hata kama haiitajiki.
g)
Wajibu
wa Mtoa Dawa katika kuchangia matumizi sahihi ya dawa
Ili kuhakikisha dawa zinatumika kwa usahihi,
Mtoa Dawa anapaswa kufanya mambo yafuatayo:-
·
Kugundua kwa usahihi dalili za ugonjwa,
·
kutoa rufaa kwa mgonjwa kwenda ngazi
inayohusika kulingana na mahitaji ya kiafya,
·
kumpa mgonjwa dawa sahihi kulingana na cheti
cha daktari au maelezo ya mgonjwa na kutoa maelekezo kwa mgonjwa juu ya matumizi
na uhifadhi sahihi wa dawa nyumbani.