Kielezo cha Usawa wa Rangi (Racial Equity Index) kilibuniwa na kikundi kilichojitolea cha watu waliotaka kugundua hali ya ukosefu na haja ya kuwepo kwa kielezo cha usawa wa rangi katika sekta ya maendeleo ya kimataifa. Utafiti huu ulibuniwa kama sehemu ya utaratibu wa utafiti wa kina wa miaka mingi unaokaguliwa wataalamu wenza na unajumuisha viashirio vya usawa wa rangi vilivyobuniwa na shirika la Racial Equity Index.
Utafiti huu utatathmini kiwango cha usawa na ukosefu wa usawa wa rangi ndani ya sekta kwa kuchunguza uwepo wake katika taasisi mbalimbali. Mbinu yake ni ya kina na inanasa viwango vingi vya usawa wa rangi na kutoa fursa ya kugundua namna nyingine za ubaguzi na ukandamizaji.
Katika utafiti wote, tunakuomba uzingatie dhana ya sehemu nyingi unapojibu maswali. Dhana ya sehemu nyingi inathibitisha kuwa watu wana vitambulisho vya kijamii vinavyohusiana vinavyoweza kujumuisha hali za kutengwa na kukandamizwa. Zaidi ya hayo, inahimiza kuwa watu wenye vitambulisho vya jamii zilizotengwa wanakabiliwa na aina na viwango tofauti vya ugumu, uwezo na haki kutokana na vitambulisho vyao.
Utafiti huu unachukua muda wa karibu dakika 20 hadi 25, na tunawahimiza wahojiwa wajaze maswali ya utafiti huu katika kikao kimoja. Tafadhali soma maagizo ya utafiti pamoja na ufafanuzi wa viashirio hapa.
Tahadhari ya Kisababishi: Tunatambua kuwa watu wengi wanaojitambulisha kama Watu Weusi, Watu wa Asili au watu wa rangi wamekumbwa na madhara, wasiwasi na unyanyasaji katika sekta ya maendeleo ya kimataifa kutokana na utamaduni wa utawala wa wazungu. Kwa hivyo, hatua ya kujibu maswali haya inaweza kuibua hisia na kumbukumbu nzito. Afya yako ni muhimu zaidi, kwa hivyo, jua kuwa si lazima ushiriki katika utafiti huu.
Kumbuka: Utafiti ufuatao, nyenzo za ziada na ripoti yoyote inayotokana na utafiti huu ni kazi halisi ya watu wa kujitolea wa shirika la Racial Equality Index na vinalindwa na hakimiliki. Hakuna sehemu ya nyenzo hizi ambayo imeidhinishwa kutolewa nakala, kuchapishwa upya au kutumika kwa makusudi yoyote bila idhini ya moja kwa moja kutoka kwa shirika la Racial Equality Index na wamiliki wa hakimiliki.
Asante kwa kuchagua kutueleza hali na maoni yako. Matokeo ya utafiti huu yatachapishwa katika ripoti kamili. Data ya utafiti itahifadhiwa na shirika la Racial Equity Index na haitatolewa nje ya shirika. Data yote iliyoripotiwa itaondolewa maelezo ya utambulisho. Tafadhali soma Sera yetu ya Faragha kwenye tovuti yetu hapa.