FOMU YA USAJILI: KAMPENI YA SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII

Kampeni hii ni huru na ya kujitolea na inahusisha watu wote watanzania wazalendo wenye moyo kutoka makundi yote ya jamii na rika lote na jinsia zote bila kujali tofauti zozote za siasa, itikadi wala imani.
Malengo ya Kampeni hii ni yafuatayo;
1. Kutambua na kutengeneza mtandao wa jamii wenye uwezo wa kupaza sauti kupinga, kupambana na kutokomeza ukatili dhidi ya Jinsia Zote Wanaume,  wanawake, watoto na wazee.
2. Kuelimisha na kurahisisha utambuzi na ufanyiwaji kazi wa viashiria vyote vya ukatilii kuanzia ngazi ya familia.
3. Kuwatambua na kuwapongeza Mashujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii waliofanikiwa kujitolea kushiriki kwenye Kampeni hii ili kuhamasisha wengine.
4. Kufikisha jumbe mbalimbali za wizara na serikali kwa ujumla kwenye jamii kupitia njia za utoaji elimu, ushirikishwaji wa wananchi kupitia makongamano.
Mfumo wa uratibu; Kutakuwa na timu za SMAUJATA kuanzia ngazi ya Taifa hadi Kijiji na zitafanya kazi kwa karibu na maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii ngazi husika kupitia kiongozi wa timu ya SMAUJATA wa eneo husika ambaye atapewa barua ya utambulisho.  Ujazaji wa fomu hii unaanza leo tarehe 28.05. 2022 na zoezi ni endelevu hadi ukatili utokomezwe nchini sambamba na Mpangokazi wa Serikali wa Kutokomeza Ukatili kwa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA 2017/18-2021/22).
Wito; Aliyeguswa na kuamua kujiunga na Kampeni hii atafuata maelekezo ya kwenye fomu ya usajili na kusubiri maelekezo zaidi.
Shukrani kwa Washiriki; kutakuwa na tuzo mbalimbali kuanzia barua, cheti, vikombe, ngao na aina zingine isipokuwa fedha. Lengo ni kuamsha ari ya uzalendo katika kupigania mambo ya msingi wa ustawi wa jamii yetu.

Sospeter Mosewe Bulugu,
Mwenyekiti wa Kampeni .
Simu +255 753 725 034
Email: Mosewesospeter70@gmail.com
Dar es Salaam.
Viongozi wa SMAUJATA baada ya kuwasilisha mfumo wa kujisajili kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Mahalumu
Email
JINA LA KWANZA *
JINA LA KATI
JINA LA MWISHO *
JINSIA *
AINA YA UTAMBULISHO *
NAMBA YA KITAMBULISHO *
NAMBA YA SIMU *
KIWANGO CHA ELIMU
Clear selection
Umewahi kupata mafunzo juu ya kupambana na vitendo vya ukatili *
Kama jibu ni NDIYO, Taja taasisi au program iliyokupa mafunzo
MKOA *
Next
Clear form
Never submit passwords through Google Forms.
This content is neither created nor endorsed by Google. - Terms of Service - Privacy Policy