Tamko la Vijana la Kusitisha matumizi ya Plastiki, linalotokana na Mkataba wa Plastiki.
Sisi, wanachama vijana wa Kuvunja Kilele cha Plastiki,Tunajiunga na wito wa kupitishwa kwa mkataba imara na wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, ukihusisha hatua za kusitisha kwa ufanisi mzunguko wa uchafuzi wa plastiki – kuanzia uchimbaji wa mafuta, Nishati isiyoendelevu, matumizi ya kemikali zenye sumu na ambazo ni hatarishi kwenye uzalishaji wake, hadi utupaji wake ambapo husababisha uharibifu mkubwa na usioepukika kwa mifumo yetu ya mazingira, wanyama wetu na afya ya binadamu. Uchafuzi unaosababishwa na plastiki kipindi chote cha maisha yake hauna mipaka na pia ni endelevu hadi vizazi vijavyo. Kama vile mabadiliko ya tabianchi. Uchafuzi wa plastiki hautishii haki zetu za binadamu tu bali mazingira safi na yenye afya endelevu, lakini pia haki za binadamu kwa kizazi kijacho. Sisi, kama vijana wa kizazi hiki, hatutaki kuishi katika sayari inayoteseka kutokana na uchafuzi wa plastiki wala kuendelea kuishi katika mazingira yenye sumu.
Sisi, vijana, ambao ni jumla ya bilioni 1.8 ya idadi ya watu wote duniani, tutakumbana zaidi na athari za uchafuzi wa plastiki. Hadi sasa wale wanaoishi kusini mwa Dunia tayari wana kabiliwa na matokeo ya mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa plastiki, na kupotea kwa bioanuai. Hata hivyo, hatuna jukumu kubwa katika mizozo hii, na bado ni kizazi chetu kinacho kabiliwa na hatari ya mustakabali ulioathiriwa sana na matokeo mabaya ya afya, majanga, nahali isiyo rafiki kuishi. Yote hayo hutokana na utegemezi wetu endelevu kwenye plastiki unaotokana na tamaa za kampuni na kutotenda kwa serikali zetu.
Sisi, kizazi kikubwa zaidi cha vijana, tumebaki na jukumu hili kubwa la kurekebisha baada ya miongo ya kupuuzwa na unyanyasaji kutoka kwa vizazi vilivyotangulia. Mgogoro wa uchafuzi wa plastiki ni moja ya changamoto kubwa zaidi ambayo kizazi chetu na vizazi vinavyofuata vinakabiliana nayo.kwahivyo, tunahitaji yafuatayo yajumuishwe katika Mkataba wa Plastiki:
Sayari yetu haiwezi kuhimili plastiki zaidi, sayari yetu haiwezi kuhimili uchafuzi zaidi. Hatuwezi kuendelea kufanya kazi kwa kutegemea rasilimali zinazo kwisha zilizo ndani ya sayari isiyo na eneo la ziada. Tunahitaji viongozi wa kimataifa kusimama katika vita hii. Tunahitaji hatua za dharura, kuingilia kati kwa nguvu, na mageuzi ya kimfumo ili kuzuia vitisho vinavyoongezeka kwa afya ya binadamu na kuvunjika kwa mifumo inayosaidia ustawi wa sayari yetu.
Proofread by Mtemi Hamisi.